NA; YOHANA CHALLE. PMT
Tanzania
inakwenda katika mashindano ya All African Game ikiwa na kumbukumbu ya
Mtanzania Bi Theresia Dismas ambaye alileta medali ya kwanza katika
ufunguzi wa mashindano hayo nchini Congo Brazzaville mwaka 1965, ambayo
kwa sasa yanatimiza miaka 50.
Shujaa
huyo kwa sasa anaishi nchini Kenya ambapo aliweza kutwaa medali hiyo
baada ya kuibuka mshindi katika zoezi la kurusha Mkuki na kuweka
historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuleta medali hapa nchini kupitia
mashindano hayo.
Hata
hivyo mwanariadha Wilhem Gidabuday alisema kuwa mashindano hayo kwa
Tanzania yana historia ya kipekee kupitia Bibi huyo na pia ni fulsa kwa
wanamichezo chipukizi kujua historia mbali mbali za mashujaa katika
michezo.
Watanzania
hasa Baraza la Michezo Tanzania (BMT),wangetumia uzalendo na upendo ili
kumjumuisha huyo mama katika Safari ya kuelekea huko Congo” alisema
Gidabuday
Aliongeza
kuwa wanariadha waliokwenda Congo Brazzaville hawajajiandaa vizuri
hivyo watanzania wasitegemee chochote kwasababu ni wanamichezo hao hao
waliotoka Nchini China katika mashindano ya Dunia na hawajapewa fulsa ya
kupumzika, hivyo kitaaluma ya michezo ni kosa.
Alisisiza
kuwa Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa katika idara ya michezo hasa
uongozi wa idara ya michezo, wengi hawana uzalendo na sio kwa upande wa
riadha pekee.
Akina
mama wengi ambao nii Viongozi wanahitaji usawa lakini sijaona
wakiumkumbuka mwanamke mwezao kwa kutoa mifano juu ya ushujaa wake
alioufanya kupitia michezo lazima wampe nafasi.
Post a Comment