PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MOMBASA WATHIBITISHA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIKAPU.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ Timu ya kikapu ya Mombasa kutoka nchini Kenya inatarajia kushiriki katika michuano ya wazi kat...
 
NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ


Timu ya kikapu ya Mombasa kutoka nchini Kenya inatarajia kushiriki katika michuano ya wazi katika mchezo huo yanayoyojulikana kama Kilimanjaro Basketball Cup yatakayofanyika Arusha kuanzia Septemba 13 hadi 19 katika viwanja vya Soweto.

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa chama cha Mchezo wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA) Barick Kilimba alisema kuwa tayari zaidi ya timu kumi kutoka ndani na nje ya nchi zimethibitisha ushiriki wao.

“zaidi ya wachezaji 100 kutoka timu  shiriki ambazo ni Soweto, Hoo,Spider, na Internatinal stars kutoka Arusha, Bandari Tanga,JKT Dar es salaam, Baptist na KCMC kutokaka Kilimanjaro, Morogoro, Zanzibar pamoja na Mombasa kutoka Nchini Kenya” alisema Kilimba

Mashindano hayo yanaandaliwa na Shirikisho la Mchezo Kikapu Tanzania (TBF) kwa kushirikiana na Chama cha mchezo wa Kikiapu Arusha (ARBA).

Kilimba alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha wanakuza mchezo huo na kuinua vipaji vipya ambavyo bado havijajulikana zaidi katika ukanda wa Kaskazini pia kutangaza vivutio vya kilatilii vilivyopo ukanda huu hasa Mlima Kilimanjaro.

“Michuano hii ilikuwa ifanyanyike Moshi lakini wenzetu wa Moshi wakatuomba ifanyike Arusha kutokana na wao kuwa na viwanja vyenye hadhi ya chini pia Mkoa huo hauna mwamko mkubwa ukilinganisha na Arusha” alisema Kilimba.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yatafunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felix Ntibenda ambaye anaonekana kupenda kukuza michezo katika mkoa wake, licha ya mashindano hayo kukosa udhamini hadi hivi sasa na kuwaomba wadau kujitokeza kudhamini mchezo huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top