Mbunge
viti maalumu CHADEMA Paulina Gekuli akiongea na wajumbe wa BAWACHA
Kiteto hivi karibuni, kulia mwenye koti jeusi ni mwenyekiti wa wilaya ya
Kiteto CHADEMA tabrani Msangi aliyesimamishwa nafasi hiyo kwa madai ya
kumnadi mgombea wa CUF kuwa Mbunge Jimbo la Kiteto
NA. Mohamed Hamad Manyara
CHAMA
cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Manyara, kimemsimamisha kazi
mwenyekiti wa wilaya ya Kiteto Tabrani Msangi, kushiriki kampeni za
uchaguzi zinazoendelea kutokana na madai kuwa amekisaliti chama na
kumnadi mgombea wa CUF kwa nafasi ya Ubunge
Hayo
yalielezwa kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho kata ya Matui siku
moja baada ya mwenyekiti wa huyo wa wilaya Tabran Msangi kumnadi
Hassani Losioki mgombea wa CUF katika mkutano ulioitwa kuwa ni wa
uzinduzi wa Ukawa mjini Kibaya
“Kuanzia
leo Tabran Msangi ni marufuku kushiriki kampeni za CHADEMA
zinazoendelea sasa kama mwenyekiti kutokana na kitendo cha kukihujumu
chama kwa kumnadi Hassan Losioki akidai kuwa ni mgombea aliyetokana na
Ukawa”alisema katibu wa CHADEMA mkoa wa Manyara
Alisema
mwenyekiti huyo toka awali alionekana kuwa msaliti, na chama kilikuwa
kinafuatilia nyendo zake na ndio maana katika hali isiyotazamiwa
alijitokeza hadharani kwenye mkutano wa CUF na kumnadi mgombea wao
Katika
kikao alichoshiriki mwenyekiti Tabrani kumnadi mgombea wa CUF alisema
CHADEMA imefanya mabadiliko ya kumteua mgombea mwingine ambaye ni Hassan
Losiok kuwa ndiye atakayepambania jimbo la Kiteto kuwa Mbunge
Alisema
mgombea Ubunge Kidawa Othman wa CHADEMA hana sifa, ana elimu ya darasa
la nne hivyo hawezi kuingia Bungeni kwa elimu hiyo na nafasi anayoiomba
ya Ubunge ni kazi kubwa ambayo kwa sasa haiwezi
Akiomba
ridhaa kwa wananchi Kidawa Othman alisema, anatosha katika nafasi hiyo
na kitendo cha kuaminiwa na chama chake ni ishara tosha kuwa anauwezo wa
kuwatumikia wananchi katika kujiletea maendeleo ya pamoja
“Siwezi
kuwa mzigo Bungeni,tumekuwa tukikosea sana kuchagua watu wenye sura ya
ukabila,uchoyo na ufisadi katika nafasi ya Ubunge ambao wamekuwa tatizo
ambalo limesababishia wananchi madhara yakiwemo ya maafa”alisema
“Tazama
tumekuwa katika mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji, hii
ilisababishwa na viongozi wetu waliolewa madaraka na kujiingiza katika
manufaa yaliyoleta madhara yakiwemo yale ya watu zaidi ya 40 kuuawa na
wengine kujeruhiwa”
Alisema
kuwa atakapochaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kuwa anaondoa ukabila
uliochimbiwa mizizi kwa watu kuchukiana kati ya wakulima na wafugaji
ambapo ilisababisha serikali kutumia fedha nyingi kuja Kiteto kufanya
uchunguzi juu ya mauaji hayo
Post a Comment