NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ
Kikosi
cha timu ya miguu ya wanawake Arusha Airtel Rising Stars walio na umri chini ya
miaka 17 kimeondoka jana (leo ijumaa) jijini hapa kikiwa na wachezaji 16
kuelekea jijini Dar es salaam katika mashindano ya Kumpata bingwa wa Mkoa
katika mashindano hayo.
Akizungumza
na gazeti hili kocha mkuu wa timu hiyo Jophrey Mlope alisema kuwa kikosi chake
kimekamilika vilivyo kwa ajili kupambana na hatimaye kuibuka washindi.
“nawahaidi
wakazi wa Arusha kuwa kikosi hiki ni imara na ninauhakika wa kurudi na ushindi,
vinaja bado wana hari ya ushindani na nimekuwa nao kwa zaidi ya wiki mbili
wakiwa wanafanya mazoezi asubuhi na jioni” alisema Mlope
“soka
la wanawake linahitaji juhudi za ziada kuanzia kata hadi taifa, japo watu wengi
wanaipa kisogo soka la wanawake na Arusha hii ina vijana wengi sana ambao
wangeweza kuinuka kupitia soka, hata ukiangalia uchaguzi wa viongozi wa soka
kwa wanawake kuna sua sua kutokana na mwamko kuwa mdogo” aliongeza kusema Mlope
Pia
alikisefu Chama cha soka Mkoa wa Arusha (ARFA) kupitia katibu mkuu Adam Brown
kwa ushirikiano wao kama chama waliouonesha kwao tangu mchakato ulipoanza na
hatimaye kupata timu
“kwangu
niwapongeze ARFA ambao wanajitahidi sana kwenye nafasi zao kama viongozi na
kama walezi, tatizo kubwa lipo kwa wadau hapa Arusha hawajitokezi kusapoti
timu, kwa sababu muda wote viongozi ndio wanajitahidi kuangalia mambo yasiende
kombo na kuna vitu vingine vilitakiwa vifanywe na wadau” alisema Mlope.
Post a Comment