PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: AFC, JKT OLJORO HAKUNA MBABE NYERERE CUP.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ Timu ya AFC inayojiandaa kushiriki ligi daraja la pili (SDL) Tanzania Bara, katikati ya wiki ...

 
NA; YOHANA CHALLE. PRINCEMEDIATZ


Timu ya AFC inayojiandaa kushiriki ligi daraja la pili (SDL) Tanzania Bara, katikati ya wiki walionesha kazi mbele ya mashabiki wao katika uwanja wa Shekh Amri Abeid walipokutana na Kaka zao JKT Oljoro na kutoshana nguvu kwa kufungana Bao 1 – 1.

Mchezo huo ulikuwa maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano yaliyoandaliwa kwa ajili ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwali Julias Kambarage Nyerere.

Oljoro ndio walikua wa Kwanza kujipatia bao kwa njia ya mkwaju wa penati kupitia mchezaji wao Lukas Charles mnamo dakika ya 62, wakati AFC walisawazisha dakika ya 78 kupitia Malechela Mndima baada ya kuitoka ngome ya Olojo.

Afisa elimu wa jiji la Arusha Josephat Ntabindi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo alipenda kuwasihi wachezaji na timu zote zinazoshirki kuhakikisha wanaanya juhudi ili kurudisha hadhi ya jiji katika michezo

“mkoa wetu unahitaji jitihada za ziada ili kuhakikisha mwakani tunakuwa na timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara,nah ii yote tutafanikiwa endapo tutashirikiana kwa pamoja” alisema Ntabindi.

Kwa sasa wakazi wa arusha wanaingalia JKT oljorokama mkombozi wao atakayewafuta aibu hiyo, Oljoro inashiriki Ligi daraja la kwanza (FDL) wakatitimu ya AFC na Mdini zikiwa zinashiriki ligi daraja la pili (SDL).

Mashondano ya Nyerere Cup yameamnadiliwa kwa lengo la Kumuenzi Mwalimu pamoja na kutangaza utalii wa ndani hasa mlima Kilimanjaro na yatafika tamati septemba 19 mwaka huu.

Bertha Ismail ambaye nimratibu mkuu wa maadhimishohayo alisema kuwa timu shiriki katika mashindano hayo, hayo ni pamoja na Nyota Accademy, Future Star, Kijenge Youth zingine ni Rolling stone, Young Life na Pallot

“Maadhimisho hayo huwa yanafanyika kila Octoba 14 kila mwaka lakini kwa mwaka huu tunafanya mwezi Septemba ili maadhimisho haya yasiathiriwe na zoezi la Uchaguzi ambapo pamoja na kumuezi Muasisi wa Taifa letu” alisema Ismail

mashindano haya pia yanahamasisha wananchi wafanye uchaguzi kwa amani bila vurugu ili sekta ya utalii hapa nchini izidi kukua.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top